0 comments
Msanii wa Rap Rosa Ree amezungumza kuhusu ngoma yake mpya aliyomshirikisha Msanii Billnas ambapo amesema kuwa aliona Billnas ndiye anafaa kwenye biti hiyo ndomana akamtumia lakini pia ni mtu wake wa karibu kwahiyo ikawa rahisi kufanya naye ngoma.
Rosa Ree amezungumzia pia kuhusu kutokufanya kazi na Management yake ya zamani ya The Industry inayomilikiwa na Navy Kenzo kama anapata changamoto zozote kwenye game ya muziki kwa sasa ambapo kataja tofauti kubwa anayoiona ni kuwa management yake ya zamani ilikuwa ni ya wanamuziki lakini ya sasa siyo wasanii.

Read More »

0 comments



 

Read More »

0 comments
Waombolezaji waliofika kumpa pole katika msiba huo.
Waombolezaji waliofika kumpa pole katika msiba huo.
Kinjekitile akitoa ufafanuzi kuhusu mazishi ya baba yake marehemu Ngombale Mwiru.
Taswira mbalimbali katika msiba huo.
Kinjekitile (kulia) akishauriana jambo na ndugu zake.

KINJEKITILE Ngombale Mwiru ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu Ngombale Mwiru ambaye amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, amesema taratibu za mazishi ya baba yao zitafanyika baada ya familia kukaa pamoja leo.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwao, eneo la Victoria, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, amewapongeza madaktari wa Hospitali ya Muhimbili kwa jitihada zao za kupigania uhai wa marehemu lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi.

“Baada ya baba kuumwa na mbwa alianza kupata complications (matatizo) ya moyo na mapafu, hivyo kwa muda wa siku tatu alihangaika sana wakati akipatiwa matibabu, hivyo cha msingi ni sisi kumwombea kwa Mungu apumzike kwa amani,” alisema Kinjekitile.


Read More »

0 comments
Kseniya wakati wa uhai wake.  Msichana huyo alikutwa akiwa amezimia kabla ya kufa akiwa katika jakuzi alilokuwa akiogea huku simu yake iliyokuwa kwenye chaji, ikiwa inaelekea kwenye maji.

Taswira nyingine ya Kseniya wakati wa uhai wake.
MWANAFUNZI mwenye umri wa miaka 12 wa kijiji kilicho karibu na  jiji la Mosow, Russia,  aliyetajwa kwa jina  la Kseniya P., hivi karibuni amekutwa amekufa bafuni baada ya simu yake (smartphone) aliyokuwa anaichaji pembeni, kutumbukia kwenye jakuzi alimokuwa  akioga.

Polisi wanaamini mtoto huyo alikuwa akisikiliza muziki wakati simu hiyo ilipoishiwa chaji na kuanguka majini,  jambo lililosababisha umeme kumfikia kutoka kwenye waya uliokuwa ukitumika kuchajia chombo hicho.

Kseniya aliyekuwa ametoka kucheza mpira wa kikapu shuleni, alifikia bafuni kuoga, lakini mama yake aliposikia ukimya bafuni, alimfuata na kumkuta tayari  kichwa chake kikiwa majini na simu ikielea kwenye maji.

Mama huyo alijaribu kuokoa maisha ya binti yake, lakini Kseniya  alikuwa tayari amekufa.

Mtoto huyo alikuwa ndiye pekee katika familia yake inayoishi kijiji cha Bolshoe Gryzlovo, wilaya ya Serpukhovsky, mkoa wa Moscow.

Read More »

0 comments


Msanii wa muziki Bongo, Mabeste amemwaga sifa lukuki kwa mke wake Lisa Fickenscher ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa (birthday).Mabeste amemueleza Lisa moja ya vitu ambavyo hajutii ni kumuoa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
Happy Birthday My Love, Sina cha kusema Zaidi ya Kusema nakupenda Saana Mama Wa Watoto wangu … Wewe Ni Mvumilivu Saaana, Unaupendo Saana, Unahuruma pia.
Kikubwa Zaidi Unaakili saaana, OooH Thanks God Kwa Zawadi Hii,
Kuna Msemo Unasema Bora Ukosee Kujenga Nyuma But Sio Kuowa, Yaniii Daah Nakupenda Saana Saaana. Kitu kingine kizuri Ulicho Barikiwa kikubwa Saana ,Unapenda Kazi Yangu ya Music Na Unajuwa Music Nzuri Ukisikia tu..Japo kuimba Ujui.
Leo ni siku Kubwa saana Kwako na Kwangu Pia..Coz Leo ndio Naachia New Track #SIJUI …Leo Mama Wa Watoto wangu Umezaliwa Upya katika Bwana Yesu ,& Hata Kipaji Changu Leo Kimezaliwa Upya Katika Jina LA Bwana wetu Yesu … Kwenye Upendo Sana Mungu Yuko Muda Wote..Coz Mungu Ni Upendo..Tutafika Safari yetu Japo Changamoto ni Nyingi..I Love u Saana.
Mabeste na mkewe, Lisa Fickenscher walifunga ndoa mwaka 2016 na hadi sasa wamejaliwa watoto wawili, Kendrick na Kaylyn.




Read More »

0 comments






Wakati kukiwa na kasumba ya wanawake kuwacheka kama sio kuwadharau wanaume wenye maumbile madogo hapa Afrika, hii ni tofauti kabisa na Roberto Esquivel Cabrera mwanaume pekee duniani anayekadiriwa kuwa na maumbile marefu zaidi ambaye anahangaika hadi leo kupata mwanamke wa kuishi naye.Roberto Esquivel Cabrera (54) raia wa Mexico amesema amekuwa akipata tabu kuchagua wanawake kwani amedai kipindi akiwa sekondari miaka 30 iliyopita wanawake wengi walikuwa wanampenda lakini kadri umri ulivyozidi kukua maumbile yake yalikuwa yanaongezeka na kuanza kumnyima raha kwani alianza kukimbiwa na wanawake.



Roberto Esquivel Cabrera

Kwenye mahojiano yake na mtandao wa IFL Science, Cabrera amesema amefanikiwa kupata mtoto mmoja tu kwenye maisha yake na mke wake wa kwanza ambaye naye alimkimbia kutokana na ukubwa wa maumbile yake.
Cabrera amesema mpaka kufikia sasa amefanikiwa kuishi na wanawake 10 lakini wote wamemuacha sababu kubwa ni kukosa furaha ya tendo la ndoa.
Nilipokuwa kijana wa miaka 20+ nilikuwa najiona mwanaume haswa kwani hata sikuwa naogopa wanawake na nilipendwa kweli lakini kadri muda ulivyozidi kwenda nikawa nahisi maumivu kwenye sehemu zangu za siri kitu ambacho kilianza kuniumiza kisaikolojia nikaanza kuwa mpweke kwani kila mwanamke niliyetaka kwenda naye faragha alinikimbia,“amesema Cabrera.
Cabrera amesema ameenda hospitali mara kadhaa akihitaji dawa za kupunguza maumbile yake lakini alichoshauriwa ni kufanyiwa upasuaji mdogo kitu ambacho hakuafikiana nacho.
Kuna watalaamu walikuja baada ya kuandikwa na vyombo vya habari wakitaka kunifanyia upasuaji nilikataa napenda niwe hivi hivi najua, kuachika na wanawake kumi hakunifanyi nikose amani najua Mungu ataniletea mwenzangu mwenye maumbile yanayoendana na yangu bado sikati tamaa,“amefunga Cabrera.
Tokeo la picha la Roberto Esquivel Cabrera
Cabrera amesema hata kama akiona amechelewa kupata mwenza nchini Mexico atasafiri hadi Marekani ambako amesema atapata wanawake wenye maumbile makubwa kwani huwa anawaona kwenye picha chafu (Video za X) na anaamini atapata mke.
Mimi nimeshakuwa mtu maarufu kutokana na maumbile yangu siwezi kuyapunguza nitaenda Marekani kule kuna wanawake wengi wenye maumbile makubwa huwa nawaona mitandaoni, siwezi kupunguza kamwe,“amesema Cabrera kwenye mahojiano yake na gazeti la The Sun la Uingereza.
Picha inayohusiana
Kwa upande mwingine Madaktari wamesema kuwa Cabrera kama angetahiriwa akiwa mdogo huenda asingelipatwa na tatizo hilo kwani linachangiwa na ongezeko la homoni.
Maumbile ya Cabrera yanakadiriwa kuwa na urefu wa nchi 18.9 hadi 20 pale yanapokuwa yamesimama na kumfanya kuwa mwanaume wa kwanza mwenye maumbile marefu zaidi duniani aliyerekodiwa.
Hata hivyo bado Cabrera hajaingizwa kwenye kitabu cha maarufu cha kumbukumbu cha (Guinness World Records). Tazama mahojiano yake hapa chini aliyowahi kufanya kipindi cha nyuma (Video by Barcroft TV).


Read More »